Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 20:16

Misri, Ugiriki na Saudi Arabia zaingia katika mazungumzo ya kuandaa Kombe la Dunia 2030


Timu ya taifa ya Saudi Aarabia.REUTERS.

Misri, Ugiriki na Saudi Arabia ziko katika mazungumzo juu ya  kuandaa kwa pamoja mashindano ya kandanda ya Kombe la Dunia 2030, afisa wa Misri alisema hivi karibuni katika matamshi  yake kwenye televisheni.

Chanzo katika Shirikisho la Soka la Ugiriki kiliithibitishia AFP mjini Athens kwamba nchi hizo tatu zilikuwa zikifanya majadiliano kuhusu kuwasilisha ombi la pamoja la kuandaa Kombe la Dunia la 2030.

Iwapo watafanikiwa, hafla hiyo itafanyika katika majira ya baridi kali ya kaskazini ili kuepuka hali ya joto kali katika nchi hizo tatu, kama ilivyokuwa kwa Kombe la Dunia mwaka huu nchini Qatar, gazeti la Uingereza la The Times liliripoti Alhamisi.

Nchi hizo tatu zinafanyia kazi kikamilifu ombi la kuandaa (Kombe la Dunia la 2030), msemaji wa wizara ya michezo Mohammed Fawzi aliiambia televisheni ya DMC.

Misri itakuwa moja ya nchi bora zaidi kuandaa hafla kama hiyo ya michezo, alisema, akisisitiza kuwa nchi yake imekuwa mwenyeji wa mashindano mengi ya ulimwengu katika miaka mitatu iliyopita.

Ombi la Misri, Ugiriki na Saudi Arabia litakuja dhidi ya angalau mapendekezo mengine mawili ya pamoja.

Argentina, Chile, Paraguay na Uruguay ziliwasilisha ombi la pamoja la kuandaa Kombe la Dunia la mwaka 2030 mapema mwezi Agosti, wakati Uhispania na Ureno zilitangaza kuandaa kwa pamoja tangu mwaka jana kuwania kuandaa mashindano hayo.

Jitihada za pamoja za Amerika Kusini zinalenga kuandaa fainali ya 2030 katika uwanja ule ule wa kumbu kumbu ya 100 huko Montevideo ambao ulikuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza ya taji hilo miaka 100 iliyopita.

Shirikisho la soka duniani FIFA linatazamiwa kuchagua mwenyeji wa mashindano hayo ya mwaka 2030 ifikapo mwaka 2024.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG