Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:42

Misri na Libya zashambulia Islamic State


Rais wa Misri, Abdel-Fattah el-Sissi
Rais wa Misri, Abdel-Fattah el-Sissi

Ndege za kivita za Misri, na Libya, zimeshambulia vituo vya kundi la Islamic State mashariki mwa Libya, Jumatatu.

Majeshi hayo yanasema mashambulizi hayo yalifanywa kulipiza kisasi kuuwawa kwa Wakristo wa Misri, 21 wa madhehebu ya Coptic.

Mashambulizi ya anga yalishambulia kambi za wanamgambo na maghala ya silaha katika maeneo ya mji wa Darba.

Majibu hayo yalifanywa saa chache baada ya kutolewa mkanda wa video unaodaiwa kuonyesha kuchinjwa kwa watu wanaodaiwa kuchukuliwa mateka nchini Libya.

Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sissi, aliapa kwenye hotuba yake katika televisheni kwamba watajibu mauaji hayo kwa kuita vitendo vya chuki vya kigaidi.

Rais El-Sissi akifuatana na mawaziri wake na alitembelea kanisa kuu la Misri na kutoa rambi rambi zake kwa jamii ya wakristo nchini humo.

XS
SM
MD
LG