Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 17:42

Misri inawanyima vitambulisho wapinzani wake waishio nje ya nchi-HRW


Human Rights Watch Logo
Human Rights Watch Logo

Maafisa wa Misri wamekuwa wakikataa kutoa kabisa vitambulisho au kuongeza muda wa vitambulisho vya wapinzani, waandishi wa habari na wanaharakati waishio nje ya nchi katika ukandamizaji dhidi ya upinzani unaoenea nje ya mipaka ya Misri, Human Rights Watch limesema leo Jumatatu.

Shirika hilo lenye makao yake hapa Marekani limesema mwaka jana liliwahoji raia wa Misri 26 wanaoishi katika nchi tofauti zikiwemo Uturuki, Ujerumani, Malaysia na Qatar, na lilipitia vitambulisho vinavyohusiana na tisa kati yao.

Kituo cha vyombo vya habari vya Misri na wizara ya mambo ya nje hawakujibu maombi ya Reuters ili kutoa maelezo kuhusu madai hayo.

“Kwa kuwakatalia kiholela raia wake wanaoishi nje ya nchi kupata pasipoti halali na vitambulisho vingine, maafisa wa Misri wanakiuka katiba na sheria za kimataifa za haki za binadamu,” Human Rights Watch imesema.

Nchini Uturuki, ambako kunaishi idadi kubwa ya wapinzani wa serikali ya Misri, Ubalozi mdogo wa Misri unawaomba wanaotafuta vitambulisho hivyo kujaza fomu zisizo rasmi na maelezo ya kibinafsi ikiwemo sababu za kuondoka Misri na akaunti zao za mitandao ya kijamii, Human Rights Watch imesema.

​
XS
SM
MD
LG