Cairo imekuwa ikishirikiana na wapatanishi wenzake mjini Doha na Washington katika miezi kadhaa ya mazungumzo kwa ajili ya sitisho la mapigano yenye lengo la kumaliza vita kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.
“Viongozi wa Hamas wametufahamisha kwamba wanachunguza pendekezo la kusitisha mapigano kwa umakini na kwa nia nzuri,”, Al-Qahera imekinuku chanzo hicho kikisema.
Chanzo hicho, ambacho hakikutajwa jina, kimesema kundi hilo la wanagambo wa Palestina linatarajiwa kujibu pendekezo hilo katika siku sijazo.
Misri, ambayo iliwaalika viongozi wa Hamas kwenye mazungumzo mjini Cairo, “ilipokea ishara zenye tija kutoka kwa Hamas ikiashiria niya yake ya kufikia sitisho la mapigano,”chanzo hicho kimeongeza.
Matamshi hayo yanajiri siku moja baada ya wawakilishi wa Hamas kukutana mjini Doha na waziri mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani na mkuu wa idara ya ujasusi ya Misri Abbas Kamel.
Forum