Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 25, 2023 Local time: 16:51

Mipango ya kumzika Gadhafi yaahirishwa.


Moammar Gadhafi

Mipango ya kumzika Gadhafi yaahirishwa kutokana na baraza la mpito kutaka eneo liwe la siri na uwezekano wa kesi katika mahakama ya lkimataifa.

Maafisa wa serikali ya muda Libya wameahirisha mipango ya kumzika kiongozi wa zamani Moammar Gadhafi leo siku moja baada ya kuuwawa baada ya wapiganaji kuvamia mji alikozaliwa wa Sirte.

Maafisa walisema mwanzo kwamba Gadhafi angezikwa Ijumaa katika eneo la siri. Hata hivyo mashirika ya habari yalikariri wanachama wa baraza la mpito la taifa (NTC) ambao wanasema mazishi yanaweza kuahirishwa kwa siku kadhaa kwa sababu ya kutokujulikana kwa eneo la mazishi na uwezekano wa uchunguzi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu.

Wakati huo huo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imetaka uchunguzi kufanyika kuhusiana na kifo cha Gadhafi. Msemaji Rupert Colville alisema hali ya jinsi gani Gadhafi alivyouwawa haijulikani na video zinazoonyesha alivyofikia kifo zinasikitisha.

XS
SM
MD
LG