Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:33

Milipuko yatingisha mji wa Maidiguri Nigeria


Police officers patrol outside the court, where suspected rioters awaited a court hearing in Kaduna, Nigeria.
Police officers patrol outside the court, where suspected rioters awaited a court hearing in Kaduna, Nigeria.

Mlipuko wa bomu huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria umeuwa watu wasiopungua wawili na kuwajeruhi wengine wanane siku moja kabla ya uchaguzi. Mlipuko wa bomu huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria umeuwa watu wasiopungua wawili na kuwajeruhi wengine wanane siku moja kabla ya uchaguzi. Mlipuko wa bomu huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria umeuwa watu wasiopungua wawili na kuwajeruhi wengine wanane siku moja kabla ya uchaguzi. Mlipuko wa bomu huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria umeuwa watu wasiopungua wawili na kuwajeruhi wengine wanane siku moja kabla ya uchaguzi.

Mlipuko wa bomu huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria umeuwa watu wasiopungua wawili na kuwajeruhi wengine wanane siku moja kabla ya uchaguzi.

Zaidi ya raia 65,000 wa Nigeria hawana makazi kutokana na ghasia ambazo zilifuatia uchaguzi wa wiki iliyopita uliomwingiza madarakani kwa mara nyingine Rais Goodluck Jonathan.

Polisi wa Nigeria wanasema mlipuko wa Jumapili ya Pasaka katika mji wa Maiduguri ni kazi ya kundi la ki-Islam la Boko Haram, ambalo limekuwa likipigana kwa miaka miwili iliyopita, ili kuunda taifa la ki-Islam huko kaskazini mwa Nigeria.

Katika taarifa iliyotolewa mapema jumapili kundi hilo lilitetea mashambulizi yake kwa polisi na viongozi wa kidini likisema wanajihusisha kimakosa na serikali kuu ambayo kundi linasema linajaribu kusambaratisha uislam

Mwanzoni mwa mwaka huu, Boko Haram lilidai kuhusika katika mauaji ya mgombea ugavana mmoja katika jimbo la Borno.

Lakini mabomu haya yanaonekana hayahusiani na ghasia za wiki iliyopita katika majimbo ya kusini ambapo wafuasi wa mgombea urais aliyeshindwa, Muhammadu Buhari, walishambulia makanisa, nyumba na vituo vya polisi, na kusababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi na wakristo.

Bwana Buhari anasema uchaguzi wa rais Jonathan uligubikwa na wizi wa kura.

XS
SM
MD
LG