Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 22:21

17 wuawa katika milipuko makanisani Garissa


Maafisa wakikagua uharibifu uliotokana na shambulizi la kigaidi katika kanisa moja Garissa Julai mosi

Polisi wawili ni miongoni mwa watu waliofariki katika mashambulizi hayo kwenye makanisa mawili tofauti

Milipuko imepiga katika makanisa mawili katika mji wa Garissa, kaskazini-mashariki mwa Kenya Jumapili, na kusababisha watu wapatao 17 kufariki na wengine 40 kujeruhiwa, wengine wakiwa mahututi, kulingana na ripoti za shirika la misaada la Msalaba Mwekundu.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Kenya polisi wawili ni miongoni mwa watu waliofariki katika mashambulizi hayo tofauti yaliyotokewa kwa wakati mmoja mjini Garissa pale watu waliofunika sura zao waliposhambulia kanisa kuu la kikatoliki na na kanisa la AIC kwa risasi na mabomu ya mkononi.

Maafisa wa serikali wa eneo hilo wamekaririwa wakisema watu wenye bunduki waliwashambulia polisi wawili na kupora silaha zao kabla ya kushambulia makanisa hayo. Miongoni mwa waliouawa pia ni wanawake sita na wanaume wengine wawili.

Majeruhi wanatibiwa katika hospitali kuu ya Garissa.

Mashambulizi ya kigaidi yamezidi Kenya tangu jeshi la nchi hiyo liingie Somalia kuwasaka magaidi wa al-Shabab Oktoba mwaka 2011.

XS
SM
MD
LG