Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:10

Zaidi ya 20 wafariki katika milipuko ya Gongo la Mboto


Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakikusanya maji kwa ajili ya wahanga wa milipuko ya Gongo la Mboto Dar-es Salaam
Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakikusanya maji kwa ajili ya wahanga wa milipuko ya Gongo la Mboto Dar-es Salaam

Maafisa wa serikali ya Tanzania wanasema takriban watu 20 wamefariki kutokana na milipuko katika kambi ya Gongo la Mboto

Maafisa wa Tanzania wanasema zaidi ya watu 20 wameuwawa usiku wa kutokana na mfululizo wa milipuko ya silaha katika kambi ya jeshi la Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Alhamisi Februari 16, 2011.

Mashahidi wanasema nyumba zilizo jirani karibu na uwanja wa ndege ziliangukiwa na mabaki kutoka nyumba nyingine pamoja na shule moja ya Sekondari.

Waziri mkuu Mizengo Pinda aliliambia bunge Alhamisi kuwa watu wapatao 145 walijeruhiwa katika mlipuko huo. Alisema watu wenmgine 4000 walokimbia makazi yao wamepatiwa hifadhi ya muda fadhi katika uwanja wa Uhuru.

Milipuko kama hiyo ikitokea kwenye kambi ya jeshi ya Mbagala mwaka 2009 na kuuwa watu wapatao 26 na kujeruhi mamia wengine.

XS
SM
MD
LG