Upatikanaji viungo

Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 20:57

Milipuko miwili ya magari yaitikisa Mogadishu, sita wauwawa


Shambulizi la mabomu karibu na ikulu ya rais, Mogadishu

Watu wasiopungua sita wameuwawa- wakiwemo washambuliaji watano – katika mashambulizi mawili Jumamosi karibu na Ikulu ya rais Mogadishu, walioshuhudia tukio hilo wamesema.

Kwa mujibu wa wale waliokuwa katika eneo hilo, gari lililokuwa linakwenda kwa kasi lililipuka kwenye kizuizi cha ulinzi karibu na bustani ya Peace Garden, eneo la umma, ikifuatiwa na milio mizito ya bunduki katika mapambano kati ya washambuliaji na majeshi ya usalama.

Habari zinasema kuwa vikosi vya usalama vilipambana na watu hao wenye silaha na kuwafurusha kutoka katika eneo la mashambulizi hayo kwenye kizuizi hicho cha ulinzi.

Ripoti za awali zinasema kuwa watu sita, akiwemo mwanajeshi wa serikali na washambuliaji watano, waliuwawa katika shambulizi hilo.

Watu wengine zaidi wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo. Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo ameiambia VOA magari ya huduma ya dharura yalifika katika eneo hilo ili kuwachukua wale wote walioumia.

Bomu jingine lililipuka katika gari ya pili karibu kabisa na eneo la Garden Peace na hoteli ya SYL, karibu na ikulu ya rais.

Hoteli ya SYL ni maarufu ambapo maafisa wa serikali hufikia hapo.

Kikundi cha al-Shabab kimedai kuhusika na shambulizi hilo la siku ya Jumamosi.

Milipuko hiyo imetokea baada ya wiki mbili ambako kulikuwa na mashambulizi kama haya katika wizara ya mambo ya ndani huko Mogadishu yaliyouwa watu wasiopungua 15.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG