Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:39

Milio ya risasi yasikika karibu na ikulu ya Guinea-Bissau


Askari wa Guinea Bissau wakiondoka kwenye mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu kijeshi huko Bissau.
Askari wa Guinea Bissau wakiondoka kwenye mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu kijeshi huko Bissau.

Milio ya risasi ilisikika karibu na ikulu ya Guinea-Bissau usiku kucha na kuendelea mpaka  Ijumaa asubuhi

Milio ya risasi ilisikika karibu na ikulu ya Guinea-Bissau usiku kucha na kuendelea mpaka Ijumaa asubuhi baada ya wanajeshi kumwachilia huru waziri kutoka chama kikuu cha upinzani aliyekuwa amekamatwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma, waandishi wa Reuters na chanzo cha polisi walisema.

Milio ya risasi ilisikika kwa mara ya kwanza usiku takriban kilomita mbili kutoka ikulu ya rais. Majibizano ya risasi yaliendelea kusikika pia baada ya saa sita usiku katika kitongoji cha Antula, nje kidogo ya mji mkuu, ambapo jenerali wa jeshi anaishi.

Milio ya risasi pia iliendelea Ijumaa asubuhi, huku magari ya kijeshi yakizunguka barabarani huku wakaazi wakielekea kazini na mashuleni.

Ofisi ya rais haina uhusiano wowote na hayo, afisa msaidizi wa mawasiliano alisema, akiongeza kuwa hakuna maoni yoyote kwa niaba yao.

Forum

XS
SM
MD
LG