Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:10

Mila ya kuwavisha majukumu vijana inavyoenziwa Kenya, Uganda


Sherehe za makabila ya Bamasaba nchini Uganda
Sherehe za makabila ya Bamasaba nchini Uganda

Sherehe za kuwavisha majukumu vijana zinazojulikana kama Imbalu, ambayo ni mila inayo heshimiwa na kuenziwa na wananchi wa Uganda na Kenya inahudhuriwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Uganda Rais Yoweri Museveni.

Mila hiyo inayothaminiwa sana kati ya makabila ya Bamasaba Mashariki mwa Uganda na Babukusu Magharibi mwa Kenya, inazinduliwa Jumamosi, Agosti 11, 2018 katika viwanja vya utamaduni vya Mutoto, Wilaya ya Mbale, Uganda.

Tukio hilo linafanyika kila Agosti ya mwaka wenye namba shufwa. Maadhimisho hayo, yatashuhudia vijana watakao pita katika mchakato huo wa kimila kufikia kuwa wametambuliwa ni wanaume wenye kuchukua majukumu katika jamii. Vijana hadi watano watakao hudhuria hafla hiyo watafanyiwa tohara katika sherehe hizo za kimila.

Tukio hilo litazinduliwa na Umukuka (chifu mkuu wa koo mbalimbali) Bob Mushikori katika viwanja vya utamaduni vya Mutoto, Uganda.

Shughuli hiyo itatanguliwa na uchangishaji fedha wakati wa chakula cha usiku katika viwanja hivyo, mchango ambao utawezesha kujengwa majengo ya kudumu yatakayo kuwa yanawakilisha koo mbali mbali za Bamasaba katika viwanja vya Mutoto.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Pheonah Wamayi Nandudu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG