Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:49

Mike Pence ajaribu kumsaidia Trump kufuatia ukosoaji wa Khan


Mgombea Makamu Rais wa Republican,Mike Pence (L) na mgombea urais wa Republican, Donald Trump.
Mgombea Makamu Rais wa Republican,Mike Pence (L) na mgombea urais wa Republican, Donald Trump.

Mgombea wa Makamu Rais wa Republican Mike Pence alisema mgombea urais wa chama hicho Donald Trump anaamini mwanajeshi muislam ambaye ni raia wa marekani aliyeuwawa na mjitoa mhanga nchini Irak mwaka 2004 ni shujaa na familia kama yake inatakiwa kuheshimiwa na kila mmarekani.

Taarifa ya Jumapili jioni inafuatia ukosoaji mkali wa majibu ya Trump kwa wazazi wa Kapteni wa jeshi la Marekani, Humayun Khan, kwenye mkutano mkuu wa Democratic wiki iliyopita. Khan aliuwawa na mjitoa mhanga nchini Irak mwaka 2004.

Mike Pence, mgombea Makamu Rais wa Republican.
Mike Pence, mgombea Makamu Rais wa Republican.

Pence alielezea haraka katika taarifa yenye maneno makali kwa Rais Barack Obama na mgombea urais wa Democratic Hillary Clinton kwa maamuzi mabaya ambayo alisema yaliruhusu kundi la Islamic State kudhibiti eneo la mashariki ya kati ambalo liliwahi kuwa thabiti.

Mike Pence na Hillary Clinton walipiga kura mwaka 2002 kuidhinisha vita nchini Irak wakiwa wanachama wa bunge la Marekani. Bwana Obama alikuwa seneta wa Illinoi wakati huo.

Taarifa ya Pence ilisema mipango ya Trump ya kuzuia wahamiaji kuingia hapa nchini umetokana na kuwepo ugaidi, kujenga tena jeshi la Marekani na kulishinda kundi la Islamic State kutazizuia familia nyingine za Marekani kutopitia kile ambacho familia ya Khan wamekipata.

XS
SM
MD
LG