Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:20

Miguna Miguna azungumza na VOA


Ghasia zilizozuka Kenya baada ya Uchaguzi wa 2007.
Ghasia zilizozuka Kenya baada ya Uchaguzi wa 2007.

Miguna 'akimbilia' Canada baada ya utata wa kitabu chake

Mwandishi wa kitabu kilichozua hisia mchanganyiko nchini Kenya Miguna Miguna, aliondoka Nairobi Jumatatu jioni kuelekea Canada ambapo anasema anakwenda kupumzika na familia yake.

Kitabu hicho kiitwacho ‘Peeling Back the Mask’ kinamshtumu na kumkosoa vikali waziri mkuu Raila Odinga. Akizungumza kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi,Miguna alisema Kenya ni nchi huru na uhuru wake pia umejikita kwenye katiba mpya ya nchi hiyo.

Akizungumzia jinsi anavyopanga kujibu wanaopinga hoja zake kwenye kitabu chake ambacho kimeibua mjadala mkali kutoka kwa wapinzani wa bwana Raila Odinga na wale wanaomuunga mkono. Bwana Miguna anasema,

“ Kenya ni nchi huru ambayo inawaruhusu raia wake hata kujiuwa wakipenda. Wakitaka wanaweza kuonyesha ujinga wao. Mimi sina haja kujibu chochote, wasome kitabu wajionee wenyewe”.

Bwana Miguna anaeleza kuwa kitabu chenyewe ni cha kurasa 588 na kwamba kimezinduliwa juzi na ana uhakika wanaoanza kumkosoa hawajapata muda hata kukisoma. Na kuhusu wanaotoa mwito wa kukamatwa kwake na kufikishwa mahakamani kwa kuficha ukweli juu ya njama anazodai kwenye kitabu hicho zilichochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliopita, Miguna aliimbia idhaa hii kuwa hilo kamwe haliwezi kufanyika.

“ Wanasema eti nikamatwe? Nikamatwe kwa kuandika kitabu? Hii itakuwa sawa na kukiuka katiba mpya ya Kenya na kurejesha nchi hii katika enzi ya utawala wa KANU.”

Miguna ambaye alikuwa mshauri wa zamani wa Bw. Odinga alisema ana haki ya kuandika kitabu hicho kinachomwelezea waziri Mkuu Raila Odinga kama mfisadi na mtu ambaye hazingatii haki.

Anadai pia kuwa mkutano wa chama cha ODM ulielezwa kuwa makabila yote 41 ya Kenya yameungana dhidi ya kabila moja. Katika mahojiano haya aliimbia sauti ya Amerika kuwa atashangaa ikiwa kitabu hiki chaweza kufanya akaadhibiwa. “ ikiwa anaweza kumnyanyasa mtu aliyekuwa mshauri wake, nini kinachoweza kufanyika endapo Raila atakuwa rais?”.

Kuhusu madai kwamba ameficha kwa muda mrefu habari ambazo pengine zingetumika kama ushahidi na wendesha mashtaka kwa mahakama ya jinai ICC kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya, kama ilivyoibuka kwamba alifahamu mengi kuhusiana na ghasia za uchaguzi uliopita, Miguna alisema hakuna mwenye uhakika ikiwa yeye amezungumza na maafisa wa mahakama hiyo ya ICC.

“ Ikiwa ICC imewaelezea Miguna amezungumzia nini au hakuzungumza, hawana hoja yoyote kusema kwamba nimeficha habari zinazoweza kutumika kama ushahidi. Je, wanajuaje sijazungumza na mahakma ya ICC?”.

Na katika mahojiano na mbunge wa chama cha ODM Bw. Ababu Namwamba, mbunge huyo aliiambia idhaa hii kuwa waziri mkuu Bw. Odinga hatajibu madai ya Miguna kwenye kitabu hicho.

Bwana Miguna alikataa kujibu swali ikiwa ana wasiwasi kuhusu maisha yake akisema kamwe hatojibu swali hilo.

Kwa hiyo kwa nini aliamua kuondoka Nairobi Jumatatu kuelekea Canada ikiwa hana wasi wasi kuhusu maisha yake?

Naenda kunadi kitabu changu na kutumia muda wanngu kukaa na familia yangu. Niko huru kama kila mtu. Niko huru kwenda katika nchi yoyote ninayotaka”.

Miguna aliskika kurekeka mno akijibu baadhi ya maswali lakini alisisitiza pia kuwa hana kesi inayomkabili huko Canada kama inavyodaiwa na hivyo hana hofu yoyote kwenda nchini humo.

XS
SM
MD
LG