Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:01

Michelle Obama awasihi Wamarekani kukemea udhalilishaji wa wanawake


Michelle Obama akizungumza kwenye mkutano wa kampeni ya Hillary Clinton
Michelle Obama akizungumza kwenye mkutano wa kampeni ya Hillary Clinton

Mke wa rais Obama, Michelle Obama alisema Alhamisi kuwa matamshi yaliyoonyesha udhalilishaji kwa wanawake na miili yao yaliyojitokeza kutoka kwa mmoja wa wagombea wa urais hapa nchini ni mabaya, machafu na yanayoumiza.

Mke huyo wa rais hakutaja jina la Donald Trump wakati akitoa hotuba iliyokuwa na msisimko kwenye kampeni yake kwa Hillary Clinton katika jimbo la New Hampshire.

Lakini alikuwa wazi akielezea shutuma kutoka kwa wanawake wanne ambao wanasema Trump aliwashika bila ridhaa yao na kuwabusu kwa lazima kwa wakati tofauti.

Michelle alisema hii sio hali ya kawaida, na hii sio siasa. Huu ni utovu wa nidhamu.

Na hii haijalishi unatoka chama gani cha kisiasa, Democratic, Republican au Independent.

Hakuna mwanamke yeyote anayestahili kupitia matukio hayo. Hakuna hata mmoja wetu anayestahili aina hii ya unyanyasaji, matukio haya yanatakiwa kusitishwa mara moja.

XS
SM
MD
LG