Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 18:03

Michelle Bachelet: Mashambulizi ya anga ya Gaza yanaweza kuangaliwa kama uhalivu wa kivita


Michelle Bachelet, Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa

Bachelet alisema hayo wakati wa kikao maalum cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kilichoombwa na Organisation of Islamic Conference, kundi la mataifa ya kiislam kutaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike kuhusu masuala ya haki za binadamu huko Israel, Gaza na ukingo wa magharibi

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet, alisema Alhamis kuwa mashambulizi ya anga huko Gaza yanaweza kuangaliwa kama uhalifu wa kivita, huku akielezea mashambulizi ya roketi yaliyofanywa na Hamas, pia yalikuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Bachelet alisema hayo wakati wa kikao maalum cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kilichoombwa na Organisation of Islamic Conference kundi la mataifa ya kiislam, kutaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike kuhusu masuala ya haki za binadamu huko Israel, Gaza na ukingo wa magharibi.

Katika maoni yaliyotolewa kutoka kwenye ofisi yake mjini Geneva, Bachelet alizungumzia mzozo wa siku 11 ambao ulimalizika kwa kusitisha mapigano wiki iliyopita. Alisema wakati mzozo ulipoanza, Hamas na makundi mengine yenye silaha yalirusha roketi kuelekea Israel. Kwa sababu mashambulizi haya hayakuwa ya kibaguzi na hayakutofautisha kati ya vitu vya jeshi na raia walifanya ukiukaji wa wazi wa kibinadamu katika sheria za kimataifa.

XS
SM
MD
LG