Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:03

Michelle Obama akumbusha utamaduni wa mwanamke wa Afrika


Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama, akizungumza kwenye kanisa la Regina Mundi wakati wa mkutano wa viongozi wanawake vijana huko Soweto, Afrika kusini, June 22, 2011
Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama, akizungumza kwenye kanisa la Regina Mundi wakati wa mkutano wa viongozi wanawake vijana huko Soweto, Afrika kusini, June 22, 2011

Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama aliwasihi vijana wanawake barani Afrika kutumia utamaduni wao wenye nguvu ili kuondokana na maovu yaliyopo hivi leo katika jamii.

Bibi Obama alizungumza kwenye mkutano uliofadhiliwa na Marekani wa viongozi wanawake vijana huko Soweto nchini Afrika kusini.
Mkutano huo umewakutanisha pamoja wanawake kutoka nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara ambao wanaongoza au wanahusika katika juhudi za kijamii na kiuchumi katika nchi zao.

Bibi. Obama aliwaambia wanawake wanawakilisha hali ya baadae barani Afrika na kwamba wao ni warithi wa damu, wavuja jasho na wahangaikaji.
Alisema kizazi chao kinaweza kuwa kizazi kimojawapo ambacho kinamaliza HIV na ukimwi. Bibi, Obama alitumia msemo uliotumika kwenye kampeni za mume wake “Ndio tunaweza” kuwahamasisha wanawake.

Mke huyo wa Rais wa Marekani aliwasili nchini Afrika kusini wiki hii. Jumanne alikutana na shujaa aliyepambana na ubaguzi wa rangi, Nelsoni Mandela mwenye umri wa miaka 92 nyumbani kwake mjini Johannesburg. Mke wa rais wa Marekani, Barack Obama alifuatana na watoto wake wawili wa kike, Malia na Sasha, mama yake mzazi, Marian Robinson pamoja na wapwa zake.

Baada ya kuitembelea Afrika kusini atafanya ziara ya siku mbili katika nchi jirani ya Botswana, anawasili nchini humo siku ya Jumamosi.

XS
SM
MD
LG