Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:00

Mgomo wahatarisha wagonjwa wa Ukimwi


Wafanyakazi wa Afrika Kusini wakiendelea na mgomo ulioingia wiki ya tatu.
Wafanyakazi wa Afrika Kusini wakiendelea na mgomo ulioingia wiki ya tatu.

Wataalamu nchini Afrika Kusini wanasema watu wengi wenye HIV huenda wakaathirika zaidi kutokana mgomo unaondelea.

Wataalamu wa afya nchini Afrika Kusini wanasema watu wengi wenye HIV nchini humo huenda wakaumwa sana na hata kufariki ikiwa ni matokeo ya mgomo ambao unawahusu wafanyakazi milioni moja nukta tatu wa kutoa huduma za umma, ikiwa ni pamoja na wauguzi na wafamasia. Wafanyakazi hao wanadai nyonyeza ya mishahara na kuboreshwa kwa mafao yao.

Hatua ya mgomo huo imefunga kliniki za serikali na mahospitali, ambayo kwa kawaida ndiyo hutoa madawa ya ARV ya kurefusha maisha ya takriban zaidi ya raia milioni moja wa Afrika Kusini walioambukizwa HIV.

Msemaji wa Wizara ya Afya nchini Afrika Kusini, Fidel Hadebe, amekiri ukubwa wa hali hiyo lakini amesema kwamba kuna machache yanayoweza kufanywa wakati ambapo kuna uhaba mkubwa wa wafanyakazi.

Mfanyakazi wa kituo cha Treatment Action Campaign (TAC) nchini Afrika Kusini, kundi ambalo linajishughulisha na masuala ya afya katika Free State, Sello Mokaliphi, amesema baadhi ya watu tayari wamefariki katika jimbo hilo kwasababu hawana fursa ya kupata madawa ya ARV.

“Bahati mbaya, kama hupo katika huduma ya kupatiwa msaada wa afya au una fursa ya kwenda kwenye kliniki binafsi kupata huduma za afya, ukweli ni kwamba watu wengi hivi sasa hawatapatiwa madawa, amesema mwenyekiti wa TAC, Nonkosi Khumalo.

XS
SM
MD
LG