Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:52

Mgomo wa mafuta Tanzania kupatiwa ufumbuzi


Wateja wanabishana wakijaribu kununua mafuta katika kituo cha Lake Oil Tabeta Sanene Tanzania
Wateja wanabishana wakijaribu kununua mafuta katika kituo cha Lake Oil Tabeta Sanene Tanzania

Wananchi wa Tanzania jumatano wameanza kushuhudia vituo vya mafuta ya petroli na dizeli vikitoa nishati hiyo baada ya kugoma kwa muda kadhaa

Tatizo la mafuta ya petroli na dizeli lililojitokeza nchini Tanzania kutokana na mgomo wa wafanyabiashara wa nishati hiyo nchini Tanzania limefanya baadhi ya wananchi kuhoji uwezo wa Serikali ya nchi hiyo wa kupambana na wafanyabiashara wanaokiuka sheria ya ushindani wa biashara.

Watu wamepanga vibuyu vya mafuta wakisubiri kuuziwa mafuta.
Watu wamepanga vibuyu vya mafuta wakisubiri kuuziwa mafuta.

Mgomo huo wa wafanyabiashara wa mafuta uliodumu kwa takriban siku saba umesababisha shida kubwa kwa wananchi lakini baada ya jumanne wabunge na mamlaka ya udhibiti wa nishati na madini- EWURA, kuchachamaa jumatano baadhi ya wafanyabiashara wameanza kutoa huduma hiyo.

Kuanzia majira ya saa tano asubuhi siku ya jumatano baadhi ya vituo vya mafuta jijini Dar es salaam vilianza kutoa huduma hiyo ya mafuta hatua iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari na watu wenye magaloni wakitaka kuwahi huduma hiyo.

Aidha wananchi wa kawaida wameitaka Serikali kuendelea kuchukua uamuzi thabiti katika matatizo mbalimbali kama hili la mafuta ili wananchi wake waweze kuendelea kuiamini.

Watu wasubiri kuuziwa mafuta.
Watu wasubiri kuuziwa mafuta.

Watu kadhaa waliohojiwa na Sauti ya Aamerika wametoa maoni tofauti na kusema kuwa inasikitisha kuona watu wanataabika na mgomo huu wa mafuta wakati ipo serikali na viongozi waliochaguliwa kuitumikia nchi.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya uhusiano na mawasiliano ya EWURA bwana Titos Kaguo jumatano alisema hali ya upatikanaji wa mafuta inaelekea kureja katika hali ya kawaida.

XS
SM
MD
LG