Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:22

Mgomo wa madereva wa malori waendelea Korea Kusini


Malori yakiwa yameegeshwa kando ya barabara kufutia mgomo wa madereva Korea Kusini
Malori yakiwa yameegeshwa kando ya barabara kufutia mgomo wa madereva Korea Kusini

Serikali ya Korea Kusini Jumanne imeamuru maelfu ya  madereva wa malori waliyopo kwenye mgomo wa kitaifa, warejee kazini, ikisema kwamba mgomo huo wa kudai malipo bora unaathiri uchumi ambao tayari unayumbayumba.

Amri hiyo ya rais Yoon Suk Yeol imeidhinishwa na bunge, wakati ikiwalenga madereva wa malori yanayobeba simenti miongoni mwa wengine. Shughuli za ujenzi kwenye maeneo mengi nchini zimesitishwa kutokana na uhaba wa simenti pamoja na vyuma, kutokana na mgomo huo.

Yeol amesema kwamba mgomo huo unatishia siyo tu uchumi wa taifa bali pia maisha ya watu ya kila siku. Ameongeza kusema kwamba hakuna sababu kamwe ya kushika mateka uchumi wa taifa pamoja na maisha ya watu kupitia malalamiko ya kundi moja.

Maelfu ya madereva wa malori ya mizigo walianza mgomo wa kitaifa Alhamisi wiki iliyopita, ukiwa wa pili kote nchini humo tangu Juni wakiitisha marekebisho ya kudumu kwenye malipo, kwa kuwa mfumo uliyopo unamalizika mwshoni mwa mwaka huu.

XS
SM
MD
LG