Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 02:40

Mgomo wa Madaktari wapamba moto Dar es salaam


Mgomo wa Madaktari wapamba moto Dar es salaam
Mgomo wa Madaktari wapamba moto Dar es salaam

Huduma za matibabu ikiwemo katika hospitali kuu ya muhimbili zimesimama kwa muda usiojulikana kufutia mzozo uliopo baina ya madaktari na serikali

Makundi ya wanaharakati pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania yamefanya maandamano ya amani na kufunga bara bara kuu katika jiji la Dar es laam kama njia ya kuishikiza serikali kuchukua hatua za haraka kutatua mzozo wa mgomo wa madaktari.

Wakati huu huduma za matibabu ikiwemo katika hospitali kuu ya muhimbili zimesimama kwa muda usiojulikana kufutia mzozo uliopo baina ya madaktari na serikali, hatua iliyofanya madaktari hao kuingia kwenye mgomo usiojulikana.


Wakiwa wamekasirishwa na hatua ya serikali kushindwa kuleta ufumbuzi hadi wakati huu, makundi hayo ya wanaharakati yameshuka barabarani na kuanzisha maandamano huku wakiwa na mabango yanayoushutumu serikali.

Baada ya kutembea hatua chache, wanaharakati hao waliweka kambi katika eneo la Daraja la Selender na kufanya mzunguko wa magari kusimama kwa saa kadhaa.

Vikosi vya usalama vilivyowasili kwenye eneo hilo kwa lengo la kuyadhibiti maandamano hayo, hata hivyo vilikabiliwa na wakati mgumu kutoka kwa wanaharakati hao, jambo lililowafanya wakune kichwa mara mbili kutafuta njia mbadala.

Wakati wote huo wanaharakati hao waliendelea kupaza sauti wakiwalalamikia viongozi wa serikali kwa kuendelea kupiga dana dana kusaka ufumbuzi juu ya mzozo huo wa madaktari.

Hii ni mara ya kwanza kwa makundi ya kutetea haki za binadamu kufanya maandamano ya amani tangu kuanza kwa mgomo wa madaktari zaidi ya wiki mbili zilizopita.

XS
SM
MD
LG