Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:13

Mgomo wa madaktari wamalizika Kenya


Madaktari nchini Kenya wametangaza kumaliza mgomo na kurejea kazini baada ya kufikia makubaliano na serikali.

kaimu wa katibu wa muungano wa madaktari nchini Kenya Chibanzi Mwachonda amesema kwamba makubaliano ya kumaliza mgomo yamefanyika baada ya rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati.

Chibanzi amesema kwamba madaktari wamerejea kazini kuanzia leo ili kuhakikisha kwamba wakenya wanasherehekea krisimasi bila kuwepo uoga wa kukosa huduma za afya.

Ameongezea kwamba mazungumzo kati ya muungano wa madaktari na serikali za kaunti Pamoja na serikali kuu yanaendelea na kufikia januari, kuhakikisha kwamba maswala yenye utata kuhusiana na maswala ya afya nchini humo yanatatuliwa.

Muungano wa madaktari hata hivyo umesema kwamba kuna baadhi ya kaunti ambazo zimeendelea kuchukua hatua ambazo sio nzuri kwa sekta ya afya nchini humo.

Waziri wa fedha Ukur Yatani, ambaye wizara yake imeshutumiwa kwa kuchelewa kutoa pesa kwa serikali za kaunti na hivyo kuchelewesha malipo ya mishahara, amesema kwamba serikali imepiga hatua muhimu sana katika kumaliza mgomo huo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG