Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:07

Kampeni za uchaguzi Marekani


Mgombea utezi wa chama cha Democratic Bernie Sanders akizungumza katika mkutano kwenye jimbo la Virginia.
Mgombea utezi wa chama cha Democratic Bernie Sanders akizungumza katika mkutano kwenye jimbo la Virginia.

Mgombea wa urais wa chama cha Demokrat, Bernie Sanders, aliwaambia wafuasi wake jana Alhamisi kuwa atafanya kazi na mgombea mtarajiwa wa chama hicho Hillary Clinton kuhakikisha Donald Trump haingii Ikulu.

Akiwa hajatangaza kumuunga mkono Clinton wala kukubali kushindwa katika kinyang’anyiro cha kugombea uteuzi wa chama Sanders alisema kumshinda Trump kwa kishindo ndio kazi kubwa ya kisiasa iliyopo.

“Hatuhitaji mgombea wa chama kikubwa anayetoa maneno ya ubaguzi kwenye kampeni yake," Seneta huyo wa Vermont alisema katika mji wa Burlington.

Alimshutumu Trump kwa kutukana Wahispania, Waislam, wanawake na wamarekani weusi, na kutoa maneno kwamba suala la kuongezeka joto joto duniani ni jambo la uongo.

XS
SM
MD
LG