Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 13:04

Mgombea Ekuru Aukot aruhusiwa na mahakama kuwania urais Kenya


Ekuru Aukot
Ekuru Aukot

Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru kwamba  mgombea urais wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot ashiriki kwenye uchaguzi wa marudio wa tarehe 26 mwezi huu.

Aukot alikuwa ameshiriki uchaguzi mkuu tarehe 8 Agosti ambao ulizua utata.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi na mipaka IEBC, ilikuwa imetangaza kwamba ni wagombea wawili pekee wangewania kwenye uchaguzi huo.

Kabla ya Aukot kwenda mahakamani, IEBC ilikusudia rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na Raila Odinga wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) ndio wanhgeshiriki kwenye uchaguzi huo wa marudio ulioitishwa baada ya mahakama ya juu nchini humo kubatilisha matokeo yaliyotangazwa ya uchaguzi wa Agosti 8.

Bw Odinga alitangaza Jumanne kwamba amejiondoa kwenye uchaguzi huo.

Baada ya uamuzi hupo wa Jumatano, Dkt Aukot alieleza kurithika kwake.

"Tunapongeza mahakama kwa sababu imekubakliana na sisi kwamba lazima katiba ilindwe..na mimi na mwenzangu Emmanuel Nzai tutashiriki katika uchaguzio wa tarehe 26," Aukot aliwaambia waandishi wa habari mjini Nairobi.

Hata hivyo, mgombea huyo, amesema bado kuna masuala ambayo chama chake kingependa yatatuliwe au kurekebishwa na tume hiyo kabla ya uchaguzi huo kufanyika.

KATIBA YA KENYA

Aukot anafahamika sana kama mmoja wa mawakili waliotayarisha rasimu ya katiba ya Kenya ya mwaka wa 2010 na baadaye kuwania urais kupitia chama cha Thirdway Alliance.

Alikuwa katibu wa kundi lililojulikana kama ‘kamati ya wataalam’ iliyotwikwa jukumu la kuweka pamoja maoni ya wakenya kuhusu mabadiliko yaliyohitajika katika katiba ya zamani iliyokuwa ikitumika tangu Kenya kupata uhuru mnamo mwaka wa1963.

Kwa wakati mmoja alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa aliamua kugombea urais ili kuzuia Kenya “kupasuliwa na ukabila na ufisadi uliokithiri.”

Alisema kwamba vuguvugu lake la Thirdway Alliance ambalo liligeuka na kuwa chama cha kisiasa, litaendelea kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter kuhamasuisha wa Kenya juu ya umuhimu wa uongozi bora usio na ukabila wala ufisadi. Alizaliwa katika Kaunti ya Turkana katika familia ya watoto 27.

Kuhusu maisha yake ya familia, Aukot alieleza kuwa baba yake alikuwa ameoa wake wengi.

Mwanasiasa huyo alizaliwa mwaka wa 1972.

XS
SM
MD
LG