Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 20:42

Trump aanza kusaka mgombea mwenza


Donald Trump

Huku mfanyabiashara tajiri, Donald Trump, akionekana kukaribia kupata uteuzi wa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan, sasa mwanasiasa huyo ameanza kutafuta mgombea mwenza kujiunga naye katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu.

Trump, ambaye hajawahi kushikilia wadhifa wa kuchaguliwa, alisema jana Jumatano kwamba anamtafuta mtu ambaye ana ujuzi wa kisiasa kuwa makamu wake wa rais.

Mwanasiasa mmoja ambaye amejiondoa mapema kwenye orodha hiyo ni Gavana wa South Carolina, Nikki Haley. Alitoa taarifa akisema atamuunga mkono Trump lakini anaangazia sana kazi aliyo nayo sasa ya ugavana.

Haley amesema "ingawa nina furaha kwamba jina langu limetajwa na ninajivunia taswira iliyopo ya mambo makubwa yanayoendelea South Carolina, nina kazi nyingi za kufanya na sina haja ya kuwa Makamu Rais."

XS
SM
MD
LG