Mgogoro wa kibinadamu kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan pia unazidisha maambukizi ikiwemo kipindupindu na magonjwa mengine yanayosababishwa na bakteria yameua zaidi ya watu 300 katika eneo hilo, afisa mmoja wa shirika la afya duniani alisema leo Ijumaa.
Afisa huyo wa WHO, Margaret Harris amesema katika mazungumzo na vyombo vya habari kwamba kuna kesi 11,327 za kipindupindu huku vifo 316 viliripotiwa na kwamba homa za msimu au Dengue, pamoja na maambukizi ya homa ya uti wa mgongo pia yaliongezeka. “Tunatarajia kuwa na kesi zaidi ya hizi zilizoripotiwa”, aliongeza.
Forum