Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:18

Mgao wa umeme utaendelea kwa muda Tanzania


Nguzo za umeme

Kamati ya bunge ya nishati na madini imewasilisha mapendekezo kwa waziri mkuu juu ya tatizo la upungufu wa umeme.

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amekaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akipendekeza kwa serikali kukodi kwa muda mitambo ya kuzalisha umeme ya Dowans ili iweze kuwashwa na kupatikana umeme

Au anasemea inabidi kutafuta kampuni binafsi itakayo nunua mitambo hiyo ili wananchi wawezi kuwa na umeme wa uhakika.Januari Makamba, mwenyekiti wa kamati ya bunge la Tanzania ya madini na nishati
Januari Makamba, mwenyekiti wa kamati ya bunge la Tanzania ya madini na nishati

Kwa upande mwengine kamati ya bunge ya nishati na madini, iliwasilisha mapendekezo yake kwa waziri mkuu siku ya Jumatano. Mwenyekiti wa kamati hiyo Januari Makamba anasema "yapo mapendekezo 30 ya muda wa dharura ya kipindi hiki cha wiki mbili, yapo mapendekezo ya muda mfupi, ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja na yako mapendekezo ya muda wa kati na ya muda mrefu".

Wananchi nao wanazidi kupaza sauti zao wakiitaka serikali kuchukua hatua za haraka kulitanzua tatizo hilo wakipinga vikali uwamuzi wa kampuni ya Dowans kulipwa fidia.

XS
SM
MD
LG