Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 16, 2024 Local time: 00:12

Mgao wa umeme kuisha Afrika Kusini


Wanaharakati wa kundi la StandUpSA na #NotInMyName wakiimba kauli mbiu wakati wakiandamana kuelekea makao makuu ya kampuni ya shirika la umeme la Eskom, mjini Johannesburg , tarehe 2, 2023 (Picha na Maria Giulia Trombini / AFP.
Wanaharakati wa kundi la StandUpSA na #NotInMyName wakiimba kauli mbiu wakati wakiandamana kuelekea makao makuu ya kampuni ya shirika la umeme la Eskom, mjini Johannesburg , tarehe 2, 2023 (Picha na Maria Giulia Trombini / AFP.

Serikali ya Afrika Kusini Jumatano iliondoa hali ya dharura ya kitaifa, ambayo ilikuwa ni hatua ya kisheria iliyoanzishwa mwezi Februari kama juhudi za haraka za kukabiliana na ukosefu wa umeme nchini humo.

Kukatika kwa umeme kumepungua katika kipindi cha wiki za hivi karibuni lakini bado unaendelea kuathiri nchi nzima ya Afrika Kusini kila siku.

"Serikali imesitisha, mara moja hali ya dharura ya kitaifa," taarifa rasmi ilisema.

Afrika Kusini imekuwa ikipambana na rekodi ya kukatika kwa umeme katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja, hali ambayo imesababisha kuongezeka kwa matatizo katika shirika la umeme la Eskom ambalo lina hali mbaya.

Mgao wa umeme ambao unahusu kukatika kwa umeme unasababisha hasara zaidi ya dola milioni 50 katika uzalishaji wa kila siku, kulingana na Waziri wa Nishati Gwede Mantashe.

Hali ya dharura kitaifa ilitangazwa na Rais Cyril Ramaphosa katika hotuba yake kuhusu hali ya kitaifa.

Siku ya Jumatano serikali ilisema tangazo hilo limeiwezesha "kuiamrisha uingiliaji kati” katika kuboresha usambazaji wa nishati.

XS
SM
MD
LG