Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 17:49

Mfumo wa malipo bila pesa walaumiwa Marekani


Mifumo ya malipo bila pesa

Mwanachama wa Baraza la Jiji la Washington, DC, David Grosso, ana amini kwamba mfumo wa malipo bila pesa taslimu, unabagua idadi kubwa ya wakaazi wa jiji ambao mfumo wao pekee wa malipo ni kwa kutumia pesa taslimu.

Grosso anataka biashara ambazo haziruhusu malipo kwa kutumia pesa taslimu kuadhibiwa.

Baraza la Jiji la Washington

Baadhi ya wanachama wa Baraza la Jiji la Washington DC wanasema kwamba mfumo wa malipo bila pesa taslimu umepiga hatua zaidi na iwapo muswada mpya wa mwanachama wa baraza hilo David Grosso utapitishwa, baadhi ya biashara ambazo hazipokei pesa taslimu huenda zikatozwa faini kubwa.

Baadhi ya wachambuzi wanadai kuwa jaribio la kukumbatia mfumo wa malipo bila kutumia pesa taslimu huenda likagonga ukuta katika jiji kuu la Washington DC.

Mfumo wa ununuzi bila ya pesa

Hata hivyo biashara nchini Marekani, kwa muda mrefu zimekuwa zikijitayarisha kwa mfumo wa ununuzi bila ya kulipa pesa taslimu na badala yake kuanza kwa matumizi ya kadi za benki.

Grosso anaeleza kuwa: “Karibu asilimia 30 ya wakazi wa jiji la Washington hawapati huduma za benki au hawawezi kunufaika na huduma za benki kwa vyovyote vile. Hii ina maana kwamba hawana akaunti za benki kabisa na hawana kadi za benki, kwa hivyo mfumo wao pekee wa malipo ni kwa kutumia pesa taslimu.”

Anaendelea kusema: “Tayari hawawezi kupata huduma kadhaa katika jamii kwa sababu hawana kiasi kikubwa cha pesa. Kwa hivyo, unapoweka masharti ya kutumia kadi za benki kwa malipo na kuondoa mfumo wa pesa taslimu, inakuwa ni makosa, na tujaribu kuzuia hilo”

Ushauri wa Grosso

Grosso anawashauri wamiliki wa biashara kununua kabati maalum ya kuweka pesa na kwamba wanaokataa kupokea pesa taslimu wanastahili kulazimishwa kulipa faini ya dola 8000. Msimamo wake unaungwa mkono na baadhi ya watu.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika anaripoti kuwa duka la Jrink, huuza juisi na vitafunio kwa watu walio katika jiji la Washington.

Jinsi mfumo huu unavyo rahisisha biashara

Unaponunua katika maduka ya Jrink, hauhitaji kusubiri salio la pesa kwani mfumo wake wa malipo sio wa pesa taslimu. Ni mfumo wa malipo kwa kutumia kadi za benki.

“Huwa tunatumia hii program ya kisasa. Bidhaa zetu zote zimo kwenye program hii kwa mpangilio wa Alfabeti na imeunganishwa kwa hii mashine ya kadi, inayosoma maelezo kulingana na mnunuzi. Unaingiza tu kadi yako unapomaliza kuagiza unachotaka, mteja anasaini halafu malipo yanafanikiswa,” anaeleza Manager wa kampuni ya Jrink, Kate Murphy.

Mfumo mwepesi kabisa

Anasema kuwa mfumo wa malipo bila kutumia pesa taslimu unafanya kazi ya wanaofanya madukani kuwa nyepesi na salama. Hamna haja kwao kuhesabu kwa mikono mapato ya siku na hakuna wasiwasi wa kuibiwa. Hivyo basi si duka la Jrink pekee linalotekeleza mfumo huu wa malipo, anafafanua Murphy.

Kwa upande wake mfanyakazi wa Jetties, Jennifer Garcia anaeleza: “kuna kampuni nilifanya manunuzi. Nilishangaa kwamba hawakua na pesa yoyote taslimu. Lakini inafanya mambo kuwa rahisi kwangu anayelipa. Napenda mfumo huu”.

Mwandishi anaeleza kuwa licha ya kuwa rahisi, mfumo wa biashara bila pesa taslimu huenda ukavunja sheria za jiji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG