Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 08, 2022 Local time: 01:03

Mfumo wa elimu Morocco umeshuka kwenye shule za umma


Mfumo wa elimu Morrocco umeshuka

Baraza kuu la elimu (CSE) limeonya kuhusu matatizo katika elimu ya umma na kusema kuwa shule za serikali haziwafundishi  wanafunzi wengi mbinu za msingi au elimu ya kimsingi

Wanafunzi katika shule za serikali nchini Moroco wanafeli na kuongeza ukosefu wa usawa, bodi ya usimamizi imeonya huku mamlaka ikihangaika kuinua ubora wa kiwango cha ufundishaji baada ya kupuuzwa kwa miaka mingi. Baraza kuu la elimu (CSE) limeonya kuhusu matatizo katika elimu ya umma na kusema kuwa shule za serikali haziwafundishi wanafunzi wengi mbinu za msingi au elimu ya kimsingi.

Licha ya msururu wa mageuzi, shule za serikali zinakuwa ndiyo nyenzo ya kuendelea kusababisha ukosefu wa usawa katika jamii, ilisema CSE katika ripoti ya mwezi uliopita, ikitahadharisha kwamba hali hii inaleta tishio kubwa. Hali hiyo imewasukuma wengi, zikiwemo familia za daraja la kati, kukazana zaidi ili waweze kulipa ada kwa watoto wao kwenda shule binafsi.

“ninalipa karibu Euro 400 kwa mwezi”, anasema Siham, mfanyakazi katika sekta binafsi. Ni nyingi, lakini ni muhimu kuhakikisha kwamba watoto wangu wawili wanapata elimu bora ya Kifaransa na Kiingereza, ambayo shule ya umma haiwezi kuwapatia.

Asilimia tisa pekee ya wanafunzi katika shule za sekondari za umma wanafaulu mitihani ya Kifaransa, Kiarabu na Hesabu, dhidi ya asilimia 62, 39, na 49 katika shule binafsi.

Abderazzak Drissi, mkuu wa shirikisho la kitaifa la waalim katika ufalme huo anasema kwamba takwimu hizi zinasikitisha, zinaonyesha kuwa tunalea raia wasiojua kusoma na kuandika.

Vitabu katika lugha tofauti ikiwemo Kiarabu
Vitabu katika lugha tofauti ikiwemo Kiarabu

Hali hiyo inatofautiana na malengo ya “New Development Model” ya Moroco yaliyowasilishwa na tume ya kifalme mwezi Mei, na kuweka malengo kadhaa ambayo yatafikiwa ifikapo mwaka 2035.

Onyo la baraza hilo ni la karibuni katika msururu wa ripoti rasmi za kuibua wasiwasi, juu ya matatizo katika mfumo wa elimu na kusababisha kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, kundi la umri lililoathiriwa sana na ukosefu wa usawa wa kijamii.

Chakib Benmoussa, ambaye alichukua wadhifa wa waziri wa elimu mwezi Oktoba nchini humo, alieleza mfumo huo unaleta maumivu. Aliliambia bunge mwezi huu kwamba, kuboresha ubora wa elimu ya umma kwanza kunategemea ubora wa mafunzo ya ualimu.

Ripoti ya CSE ilikubali na kuongeza kuwa wengine huchagua taaluma hiyo kwa ukosefu wa njia mbadala.

Kulingana na takwimu za wizara, mwaka huu zaidi ya waombaji laki moja waliomba kazi za ualimu zisizozidi 17,000.

Chini ya Benmoussa, wizara imeleta sharia mpya zinazohitaji waalim watarajiwa kuwa na umri wa chini ya miaka 30, na kuwa na shahada ya chuo kikuu chenye kiwango. Lakini ingawa kuna makubaliano juu ya matatizo haya maoni yanatofautiana juu ya suluhisho.

Masharti hayo mapya yalizua taharuki kutoka chama cha waalimu, na waalimu wanaopatiwa mafunzo, huku kuki-ibuka maandamano ya mitaani mwezi uliopita.

Drissi, mwanachama wa chama cha waalimu alisema kwamba kinachohitajika ni mtihani mgumu zaidi wa kuingia, sio umri. Lakini afisa huyo wa wizara alisema kuwa kwa sasa ni muhimu kurekebisha mfumo wa elimu. Tumechelewa sana”.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG