Ray Hunt, ambaye ana majina mwengine - Abdolrahman Hantoosh, Rahman Hantoosh au Rahman Natoosh – anadaiwa kuuza Iran mafuta na gesi, pamoja na vifaa vya viwandani kupitia kwa kampuni yake ya Alabama.
Ili kuheba vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran, Hunt anadaiwa kusafirisha vitu hivyo kupitia Uturuki na umoja wa falme za kiarabu.
Hunt anadaiwa kukula njama za kuilaghai serikali ya Marekani, kukiuka vikwazo, kusafirisha bidhaa kwa njia ya magendo kutoka Marekani na kutoa habari za uongo na za kupotosha kuhusu bisahara yake.
Mshukiwa, mwenye umri wa maiak 69, Mmarekani mwenye uraia wa Iran, amefikishwa mahakamani, Alabama, jana Jumanne.
Endapo atapatikana na makosa, anaweza kufungwa hadi miaka 20 gerezani na kulipa faini ya dola milioni 1 kwa kukiuka vikwazo vya kibiashara vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran. Isitoshe, anakabiliwa na hukumu ya hadi miaka 5 y aulaghai, miaka 10 ya biashara ya magendo, na miaka 5 ya kutoa habari za uongo.