Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:36

Mfalme wa Zulu Goodwill Zwelithini afariki


Mfame Goodwill Zwelithini ( katikati) kwenye picha ya awali.
Mfame Goodwill Zwelithini ( katikati) kwenye picha ya awali.

Kiongozi wa kitamaduni wa kizulu wa Afrika kusini mfame Goodwill Zwelithini amefariki Ijumaa kiwa na umri wa miaka 72 baada ya kuugua kwa zaidi ya mwezi mmoja kulingana na ripoti kutoka kwa familia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Zwelithini amekuwa akikabiliana na maradhi ya kisukari kwa muda sasa. Zwelithini ambaye ni mfalme wa nane wa jamii wa Zulu ametawala kwa zaidi ya miaka 50, na kwa hivyo kufanyika kuwa kiongozi iliyedumu kwa muda mrefu zaidi.

Ingawa kama kiongozi wa kitamaduni hakua na ofisi ya kisiasa, Zwelithini alikuwa mwenye ushawishi mkubwa miongoni mwa wa Zulu takriban milioni 12, ambao ni kabila kubwa zaidi Afrika kusini, lenye jumla ya watu milioni 60.

Zwelithini amekuwa mkosoaji mkubwa wa mpango wa serikali wa kugawa ardhi ambao ungeathiri maeneo makubwa ya ardhi yanayomilikiwa na watu wa Zulu. Hisani ya Ingonyama Trust iliyoongozwa naye inamiliki asilimia 29 ya ardhi kwenye mkoa wa KwaZulu -Natal ikiwa na ukubwa wa kilomita 28,000 mraba.

Watu wa kabila la Zulu chini ya uongozi wa mfalme Shaka Zulu walipigana vikali na wakoloni wa Uingereza kati ya mwaka wa 1816 na 1828.

Imetayarisha na Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG