Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 12:33

Meya wa New York City awataka watu kuwa na subra za taarifa ya shambulizi


Meya wa New York City, Bill de Blasio.
Meya wa New York City, Bill de Blasio.

Meya wa mji wa New York City, Bill de Blasio alisema watu watatakiwa kuwa na subra ili kupata taarifa kamili kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea jumamosi usiku katika eneo la Manhattan ambalo liliwajeruhi watu 29 katika moja ya miji yenye harakati nyingi jimboni humo.

Alisema tuna kazi zaidi ya kufanya ili kuweza kusema kile kilichochochea tukio hili kufanyika. Je lilichochewa kisiasa, au ni kuhusiana na uamuzi binafsi, lakini maswali yote haya bado hayana majibu.

Wakati huo huo ofisa mmoja wa usalama ameliambia shirika la habari la Associated Press-AP kwamba wachunguzi hawaweki umakini mkubwa wa madai ya uwajibikaji yaliyosambazwa kwenye tovuti ya mtandao wa kijamii ya Tumblr. Hata hivyo tovuti hiyo iliondoa tangazo hili na haijatoa matamshi yeyote. Gavana wa New York, Andrew Cumo alisema mlipuko huo ulikuwa kitendo cha ugaidi lakini hakuna ushahidi wa ugaidi wa kimataifa.

XS
SM
MD
LG