Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:11

Meya wa Harare aeleza wasi wasi juu ya upatikanaji umeme wakati wa sikukuu


Rais wa Zimbabwe Mnangagwa alipozungumza na wananchi Jumatatu ya Aug. 13, 2018.
Rais wa Zimbabwe Mnangagwa alipozungumza na wananchi Jumatatu ya Aug. 13, 2018.

Ili kuuhamasisha msimu wa sherehe, meya wa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, hivi karibuni aliwasha taa za Krismasi katikati ya jiji. Lakini kwa wengi, tukio hilo lilikuwa ni ukumbusho wa mambo mawili wanayotamani lakini hawawezi kuyapata: umeme na kipindi cha likizo ya furaha.

Hata Meya Jacob Mafume hakuonekana kuwa na imani kwamba mji mkuu utashuhudia Krismasi iliyong’aa.

Tunatumai umeme utaendelea kuwepo wakati wa msimu wa sikukuu," alisema katika hafla ya kuwasha taa ya mti wa Krismas, ambayo miaka ya nyuma imekuwa na hali ya furaha. "Angalau leo tunao umeme na tunatumai kuwa kwenda mbele taa hazitazimika.”alisema.

Huku tishio la COVID-19 likiwa linapungua, Zimbabwe imelegeza vikwazo vya usafiri na mikusanyiko. Lakini hali nzuri ya likizo isiyo na mvuto haiinui nchi ambayo pia inakabiliana na mfumuko wa juu wa bei za vyakula ulimwenguni.

Bei za vyakula zimepanda Ulimwenguni kutokana na vita vya Ukraine na Wazimbabwe wameathirika vibaya sana. Taifa hili la kusini mwa Afrika lenye watu milioni 15 ndilo linaloongoza kwa mfumuko wa bei za chakula duniani, kwa asilimia 321, kulingana na taarifa ya usalama wa chakula ya Benki ya Dunia mwezi Desemba.

XS
SM
MD
LG