Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 23:30

Mexico yasema imekubaliana na Marekani katika mazungumzo ya kudhibiti wahamiaji


Maafisa wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka wa Marekani wakimchukua mtoto wa mhamiaji kutoka kwa mama yake baada ya kuvuka mpaka huko Eagle Pass, Texas Desemba 22, 2023. Picha na AFP
Maafisa wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka wa Marekani wakimchukua mtoto wa mhamiaji kutoka kwa mama yake baada ya kuvuka mpaka huko Eagle Pass, Texas Desemba 22, 2023. Picha na AFP

Mexico inasema imefikia makubaliano muhimu na Marekani baada ya mazungumzo yenye lengo la kuzuia mtiririko wa wahamiaji.

Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alikutana na Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador siku ya Jumatano katika mashauriano ya faragha.

Kwenye mtandao wa kijamii, Lopez Obrador alisifu kile alichokielezea kama makubaliano muhimu lakini hakutoa maelezo.

Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani mapema mwezi huu ilifunga kwa muda vivuko viwili muhimu vya reli kati ya Texas na Mexico, na kufunga vivuko vingine, ili kukabiliana na msongamano mkubwa wa wahamiaji.

Waziri wa mambo ya nje Alicia Barena alisema Mexico ilitaka vivuko hivyo vifunguliwe tena.

Lopez Obrador wiki iliyopita aliihakikishia Marekani kwamba Mexico itasaidia kupunguza shinikizo la wahamaji.

Mapema Jumatano, alisema Bunge la Marekani linapaswa kuwekeza kwa watu maskini huko Amerika Kusini na Caribbean badala ya kufikiri juu ya kujenga ukuta.

Rekodi ya idadi ya watu wanaokimbia uhalifu, umaskini, na migogoro na kufika kwenye mpaka wa Marekani, ni suala muhimu kabla ya uchaguzi wa rais wa Novemba.

Rais Joe Biden anataka Mexico imsaidie kupunguza idadi hiyo, kabla ya azma yake ya kuchaguliwa tena.

Forum

XS
SM
MD
LG