Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:43

Mexico yaokoa wahamiaji 31 waliotekwa


Serekali ya Mexico imewaokoa wahamiaji 31, wakiwemo wanawake na watoto, waliotekwa mwishoni mwa juma katika jimbo la kaskazini mwa Mexico la Tamaulipas, maafisa walitangaza Jumatano.

Msemaji wa rais Jesus Ramirez, alithibitisha uokoaji huo kwenye mtandao wa kijamii wa X, zamani Twitter.

“Tayari wapo mikononi mwa mamlaka na wanaendelea na uchunguzi wa kimatibabu unaostahili,” aliweka pamoja na picha iliyowaonyesha wanaume, wanawake na watoto.

Wahamiaji hao walikuwa salama na wenye afya njema, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Mexico, Luisa Alcalde aliandika kwenye mtandao wa X, akinukuu habari kutoka kwa gavana wa jimbo hilo.

Watu wenye silaha waliwateka wahamiaji hao Jumamosi kutoka katika basi kwenye barabara kuu katika manispaa ya Reynosa, karibu na mpaka wa Mexico na Marekani.

Basi hilo lilikuwa likielekea Matamoros, ng'ambo ya Brownsville, katika jimbo la Marekani Texas.

Forum

XS
SM
MD
LG