Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 02:55

Mexico yaanza kurejesha wahamiaji nchini Haiti


Wahamiaji kutoka Haiti wakipanda ndege kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa waVillahermosa, Mexico, Septemba 29, 2021.
Wahamiaji kutoka Haiti wakipanda ndege kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa waVillahermosa, Mexico, Septemba 29, 2021.

Mexico Jumatano ilianza kurejesha wahamiaji wa Haiti nchini mwao ikianza na kundi la kwanza la watu 70 hadi kwenye mji mkuu wa Port au Prince.

Ndege ya kwanza imeondoka Jumatano kutoka uwanja wa ndege wa Villahermosa kwenye jimbo la Tabasco ikiwa imebeba wahamiaji 41, kumi na sita wakiwa wanawake na watoto 13.

Idara ya uhamiaji ya Mexico imesema kwamba wahamiji hao wanarejeshwa kwa hiari yao.

Idara hiyo pia iliashiria kwamba safari ya Jumatano huenda ikawa mwanzo wa kuwarejesha maelfu ya wahamiaji wa Haiti ambao wamekwama kwenye mpaka wa Mexico na Marekani mwezi huu.

Maelfu wengine wamekwama kwenye mji wa kusini wa Tapachula karibu na mpaka wa Guatemala wakati wakisubiri majibu kutokana na maombi yao ya hifadhi nchini Mexico kutoka kwa maafisa wa uhamiaji wa taifa hilo.

Ijumaa wiki iliyopita, rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador alisema kwamba hawatakubali Mexico "kuwa kambi ya wahamiaji" na kuongeza kwamba ni wakati wa kushughulikia tatizo hilo.


XS
SM
MD
LG