Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:05

Kiongozi wa Mexico akataa kulipia gharama za ujenzi wa ukuta


Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto.
Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto.

Rais wa Mexico anafikiria kufutilia mbali ziara aliyoipanga kuifanya Washington wiki ijayo kufuatia amri ya Rais Donald Trump kuwa ujenzi wa ukuta kati ya nchi hizo mbili uanze mara moja, amesema msemaji wa ngazi ya juu.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni kwa taifa Jumatano, Rais Enrique Pena Nieto amesema anasikitishwa na hakubaliani na uamuzi wa Marekani, na amerejea tena kusema kwamba Mexico haitolipa gharama za ujenzi wa ukuta huo pamoja na Trump kutoa kauli hiyo.

“Mexico haiamini katika kuweka ukuta, “alisema rais huyo. “Nimesema mara nyingi, Mexico haitalipa gharama zozote za ujenzi wa ukuta.”

Pena Nieto hakusema moja kwa moja kuhusu safari yake, lakini akagusia kuwa atangojea ripoti kutoka kwa maafisa wa ngazi ya juu wa Mexico ambao hivi sasa wanakutana na uongozi wa Trump huko Washington.

“Ikitegemea ripoti ya mwisho kutoka kwa viongozi wa Mexico ambao wako Washington hivi sasa… Nitafanya uamuzi kipi cha kufanya baada ya hapo,” amesema.
Baada ya kuonyesha msimamo mkali kuhusu ukuta huo, alishika tawi la mti wa mzeituni akisema “Mexico inaahidi tena kuendeleza urafiki na watu wa Marekani, na nchi yake iko tayari kufikia makubaliano na serikali yao.

Hasira imeongezeka Mexico

Uamuzi wa rais huyo kufikiria tena uwezekano wa kutembelea Marekani umekuja wakati wananchi wa Mexico wakiwa na hasira, na kuhisi kuwa Pena Nieto ameonyesha udhaifu katika kukabiliana na sera za ubabe za Trump.

Afisa ambaye hana mamlaka ya kulizungumzia suala hili na hakutaka jina lake litajwe, ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa utawala wa Mexico “unatathmini” iwapo ziara hiyo ya Januari 31 isiwepo. “Hilo ndilo ninaweza kusema.” Haikuwa wazi ni lini uamuzi huo wa mwisho juu ya ziara hiyo utafanyika.

Lakini agizo la Trump lilikuja siku ambayo Mawaziri wa Mexico wa mambo ya nje na uchumi walipowasili Washington kwa mazungumzo na uongozi wake, na uwepo wao ulionekana na watu wa Mexico kama udhalilishaji.

Kushuka umaarufu wa Pena Nieto

Wapinzani wa Pena Nieto, ambaye kiwango cha kukubalika kwake kimeshuka kufikia asilimia 12 katika tafiti za hivi karibuni, ambacho ni chini kuliko rais yeyote wa Mexico katika kura za maoni za zama zao—wamemshutumu kwa udhaifu aliyouonyesha katika kupambana na Trump. Wanasiasa wa kambi ya upinzani wamemhimiza Jumatano kufutilia mbali ziara yake Marekani.

“Msimamo uko wazi,” amesema Ricardo Anaya Cortes, rais wa chama cha wconservative wa upande wa upinzani cha National Action Party.

“Ni kati ya mambo mawili, afutilie mbali mkutano na Donald Trump, au ashiriki ili amweleze wazi na bila ya kutetereka kwamba Mexico inakataa ukuta huo na haitolipa hata senti moja kwa ajili ya ujenzi wake.”

XS
SM
MD
LG