Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 05:41

Kemikali ya Methanol yalaumiwa kwa vifo vya vijana Afrika Kusini


Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa akiongoza waombolezaji kwenye mazishi ya vijana waliokufa kwenye klabu mwezi Juni
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa akiongoza waombolezaji kwenye mazishi ya vijana waliokufa kwenye klabu mwezi Juni

Daktari Litha Matinawe ambaye ni naibu mratibu wa huduma za afya kwenye jimbo la Eastern Cape , Afrika kusini, amesema kwamba ripoti ya kilichosababisha vifo vya vijana hivi karibuni imetolewa.

Matinawe amesema hayo Jumane wakati akiongea na wanahabari kwenye mji wa East London, kwamba kemikali hatari aina ya methanol huenda ilisababisha vifo vya vijana 21 kwenye mji huo mwezi uliopita. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, kemikali hiyo ilipatikana kwenye kila mwili wa waathirika hao baada ya kufanyiwa uchunguzi ,wakati wataalam wakiendelea kubaini iwapo viwango vilivyopatikana vilitosha kusababisha vifo hivyo.

Vijana hao ambao wengi walikuwa wanafunzi walikufa wakati wakiwa ndani ya klabu kimoja cha usiku mjini humo. Methanol ni kemikali yenye uwezo wa kulevya na ambayo hutumika kwenye viwanda au kutengeneza dawa za wadudu, na wala sio pombe ya kutumiwa na wanadamu.

Vijana hao waliokuwa na umri kati ya miaka 13 na 17 walipatikana wakiwa wamekufa kwenye klabu hiyo, miili yao ikiwa imetapakaa kila mahali. Polisi wa Afrika kusini wanasubiri matokeo kamili ya uchunguzi, ili kubaini ni nani atakaye funguliwa mashitaka kutokana na mkasa huo wenye kusikitisha.

XS
SM
MD
LG