Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:23

Messi ahukumiwa miezi 21 jela


Mchezaji mpira mashuhuri duniani Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 nchini Spain baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kulipa kodi. Baba yake, Jorge Messi, pia alipewa hukumu ya kifungo gerezani kwa kosa la kukwepa kodi kiasi cha paundi millioni 3.5 hadi 4.5 kati ya mwaka 2007 na 2009.

Wote wawili wanakabiliwa pia na faini ya mamillioni ya Euro kwa kutumia nchi za belize na Uruguay kuficha mapato yao kwa nia ya kukwepa kodi.

Hata hivyo, Messi na baba yake hawatazamiwi kutumikia adhabu hizo gerezani

Kulingana na sheria za Spain, kifungo cha chini ya miaka miwili kinaweza kutumikiwa kama kifungo cha nje.

XS
SM
MD
LG