Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:39

Meriam Yahya Ibrahim akutana na Papa Francis


Meriam na mwanaye Maya wakiwa Vatican na Papa Francis, July 24, 2014.
Meriam na mwanaye Maya wakiwa Vatican na Papa Francis, July 24, 2014.

Jaji moja wa Sudan alimhukumu kifo mama huyo mwezi Mei kwa kukataa kukana imani yake ya Kikristo. Kwa mujibu wa sheria za Sudan, watoto wa wanaume waislam wanategemea kuwa waislam. Meriam alilelewa na mamake mkristo.

White House inasema ina furaha kuu kwamba mwanamke raia wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kukataa kukana imani yake ya kikristo yuko salama na kwamba yuko njiani kuja Marekani.

Meriam Yahya Ibrahim aliwasili Roma Italia Alhamisi pamoja na mume wake na watoto wadogo wawili ikiwa ni pamoja na mtoto wa kike mchanga aliyezalia jela huko Sudan.

Muda mfupi baada ya kuwasili Meriam na familia yake walikutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis. Msemaji wa Vatikan alisema Papa Francis alimshukuru Meriam kwa imani yake na ujasiri wake.

Susan Rice, mshauri wa maswala ya ulizni wa kitaifa Marekani, alisema Marekani itapata nguvu za kutetea uhuru wa kidini kwa kutumia mfano wa Meriam Ibrahim wakati inapotetea wale wanaonyimwa haki hizo .

Jaji mmoja wa Sudan alimhukumu kifo mama huyo mwezi Mei kwa kukataa kukana imani yake ya Kikristo.Kwa mujibu wa sheria za Sudan,watoto wa wanaume waislam wanategemea kuwa waislam. Meriam alilelewa na mamake mkristo.

Mwezi jana mahakama ilifutilia mbali hukumu yake ya kifo na Meriam na familia wakatafuta hifadhi katika ubalozi wa Marekani mjini Khartoum.

XS
SM
MD
LG