Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:39

Meli ya kwanza iliyobeba nafaka yaondoka kufuatia makubaliano na Russia


Meli iliyobeba nafaka iliyoruhusiwa na Russia kuondoka bandarini, mjini Odesa, Ukraine. Oleksandr Kubrakov/ Ukraine Ministry of Infrastructure/Handout via REUTERS
Meli iliyobeba nafaka iliyoruhusiwa na Russia kuondoka bandarini, mjini Odesa, Ukraine. Oleksandr Kubrakov/ Ukraine Ministry of Infrastructure/Handout via REUTERS

Maafisa wa Ukraine na Uturuki wamesema ikiwa ni safari ya kwanza tangu Russia walipoivamia Ukraine na kuzuia usafirishaji kupitia Black Sea miezi mitano iliyopita.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine ameiita “siku ya nafuu kwa dunia,” hasa kwa nchi zilizotishiwa na uhaba wa chakula na njaa kwa sababu ya kuvurugika kwa usafirishaji wa nafaka.

Safari hiyo iliwezekana baada ya Uturuki na Umoja wa Mataifa kusimamia makubaliano ya kusafirisha nafaka na mbolea kati ya Russia na Ukraine mwezi uliopita katika makubaliano nadra ya kidiplomasia kwenye mzozo ambao unaendelea huku kukiwa hakuna suluhu katika eneo la tukio.

Tume ya Ulaya imekaribisha safari hiyo.
Peter Stano, msemaji wa tume ya ulaya anaeleza: "Jumuiya ya Ulaya imekaribisha kuondoka kwa meli ya kwanza ya kibiashara kutoka bandari ya Odesa kufuatia makubaliano ya juhudi za nafaka kupitia Black Sea ya Julai 22, baada ya kuzuiliwa kwa miezi kadhaa wakati Russia ilipolenga bandari hii siku moja baada ya kuweka sahihi.

Hii ni meli ya kwanza ya kibiashara kuondoka bandari ya Black Sea ya Ukraine tangu uchokozi wa Russia kuivamia Ukraine Februari 24 na kuzuiliwa bandari za Ukraine na usafirishaji nje wa nafaka. Na hii ni hatua ya kwanza kukaribishwa kupunguza mzozo wa chakula duniani uliosababishwa na uchokozi haramu wa Russia dhidi ya Ukraine na kuzuiwa bandari za Ukraine pamoja na madini, kuharibu mashamba Ukraine, kuchoma nafaka na ngano au kuiba na kujaribu kuuza kwa niaba yake.”

Inategemewa kwamba makubaliano hayo yatarahisisha mzozo wa chakula duniani na kupunguza gharama za nafaka.

XS
SM
MD
LG