Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:39

Miale ya chombo cha mawasiliano cha ndege ya EgyptAir imepatikana


Meli ya kivita ya Ufaransa kwa kutumia vifaa vya kunasa miale chini ya bahari imeweza kupata miale kutoka wa chombo cha kunasa habari cha ndege ilioanguka ya Egypt Air baada ya kupoteza mawasiliano ya radar Mei 19 wakati ikielekea Cairo kutoka Paris na kuuwa abiria wote 66 waliokuwa ndani.

Chombo hicho maarufu 'black box' kinaaminika kuwa chini ya bahari ya Mediterranean kati ya kisiwa cha Ugiriki cha Crete na ufukwe wa Misri.

Tangu mkasa huo ulipotokea, wachunguzi hawajaweza kubaini kiini chake. Vile vile, hakujakuwa na kundi lililodai kutekeleza ajali hiyo ya ndege aina ya Airbus A-320.

XS
SM
MD
LG