Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 11:09

Melania Trump kuzuru baadhi ya nchi za Afrika


Mke wa rais wa Marekani, Melania Trump.
Mke wa rais wa Marekani, Melania Trump.

Mke wa rais Donald Trump wa Marekani, Melania Trump, atazuru bara la Afrika baadaye mwaka huu. Hata hivyo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, ratiba rasmi ya ziara hiyo haikutolewa mara moja.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Bi Trump kuzuru bara hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na afisi ya Bi Trump, mke huyo wa rais anatazamia kujifunza kuhusu changamoto zinazowakabili watoto wa bara hilo.

“Ni wazo la kusisimua kwamba nitazuru Afrika na kujifunza kuhusu masuala ya watoto tamaduni na historia za bara hilo.”

Rais Donald Trump hajazuru bara hilo tangu aingie madarakani na ameshutumiwa kwamba alitoa maneno ya matusi mapema mwaka huu, yaliyoelekezwa kwa nchi za bara hilo.

Melania Trump hata hivyo amesema kwamba anaamini utengamano duniani ni muhimu na kwamba mazungumzo kati ya jamii mbalimbali yana manufaa makubwa kwani “yanachangia katika mchakato wa kujifunza kutoka kwa jamii mbalimbali.”

Msemaji wa Bi Trump, Stephanie Grisham, amesema kwamba White House itatoa ratiba rasmi na orodha ya nchi atakazotembelea katika wiki chache zijazo.

XS
SM
MD
LG