Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:09

Melania Trump 'hakuiba' hotuba ya Michelle Obama - Warepublikan


Melania Trump akitoa hotuba yake Jumatatu usiku
Melania Trump akitoa hotuba yake Jumatatu usiku

Mwenyekiti wa kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican, Paul Manafort anakanusha madai kuwa mke wa Trump, Melania, aliiba maneno kutoka hotuba Michelle Obama katika hotuba yake kwenye siku ya kwanza ya mkutano mkuu wa uteuzi wa chama cha Republican Jumatatu usiku.

Mkutano huo umeingia siku ya pili Jumanne huku ukitazamiwa kutilia mkazo maswala ya uchumi, lakini gumzo kubwa katika vyombo vya habari limekuwa hotuba ya Melania Trump ambayo ilikuwa na sehemu zilizofanana neno kwa neno na hotuba aliyotoa Michele Obama mwaka 2008.

Melania Trump
please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:00:58 0:00

Melania aliwaeleza watazamaji kwamba mume wake Donald Trump ni kiongozi mwenye sifa na ndie pekee anayeweza kuleta mabadiliko kwa Marekani. Wazungumzaji wa Jumanne huko Cleveland katika jimbo la Ohio ni pamoja na baadhi ya viongozi muhimu wa chama akiwemo spika wa bunge Paul Ryan na wagombea wa zamani wa urais, Chris Christie na Ben Carson. Katika hotuba yake Jumatatu usiku, Melania Trump aliongeza kusema kama unamtaka mtu wa kukupigania wewe na nchi yako, ninakuhakikishia kwamba huyu ndie mtu anayestahiki, akimaanisha Donald Trump.

XS
SM
MD
LG