Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 15:07

Melania Trump amemtetea mumewe dhidi ya kadhia ya ngono


Melania Trump na mumewe Donald Trump, kwenye mkutano mkuu wa Republican. July 18, 2016.
Melania Trump na mumewe Donald Trump, kwenye mkutano mkuu wa Republican. July 18, 2016.

Mke wa mgombea urais Marekani wa chama cha Republican, Donald Trump, bi. Melania Trump alimtetea mume wake kufuatia shutuma zilizosambaa kwenye vyombo vya habari juu ya namna mume wake alivyojigamba kwa mtangazaji wa televisheni juu ya jinsi alivyo wavamia kingono wanawake bila ya idhini yao.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN cha Marekani jumatatu usiku, Melania Trump alieleza kwamba mume wake alishinikizwa na mtangazaji wa televisheni wa kipindi cha “Access Hollywood”, Bill Bush kusema maneno ya kudhalilisha wanawake yaliyorekodiwa kwenye video mwaka 2005.

Aliongeza kusema matamshi aliyosikia yanatoka kwa mwanamume asie mumewe anaemjua. Akimsifu kua ni mtu mnyenyekevu na anafahamu ni mtu anaeheshimu wanawake. Anasema Trump ameshaomba msamaha kwa umma kufuatia matamshi hayo huku akisisitiza kwa lugha nyepesi hayo yalikuwa mazungumzo ya “wavulana”.

XS
SM
MD
LG