Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 05:00

Megrahi afariki kutokana na saratani


Abdelbaset Ali al-Megrahi, akiwa katika siku zake za mwisho baada ya hali yake ya afya kuzorota haraka.
Abdelbaset Ali al-Megrahi, akiwa katika siku zake za mwisho baada ya hali yake ya afya kuzorota haraka.

Abdel Baset al-Megrahi, afisa wa zamani wa ujasusi wa Libya aliyehukumiwa kwa kulipua bombu ndani ya ndege ya Pan Am 1988 amefarikiamjini Tripoli.

Al-Megrahi alifariki nyumbani kwake Jumapili, akiwa na umri wa miaka 60. Yeye ni mtu pekee aliyepatikana na hatia ya kushambulia ndege ya Pan Am 103 ilipokua inaruka kupitia Lockerbie, Scottland, na kusababisha vifo vya abiria wote 270 na watu 11 walokua nchi kavu.

Afisa huyo wa zamani alipatikana na hatia mwaka 2001, ya kuhusika katika njama ya kulipua ndege hiyo, miaka miwili baada ya kiongozi wa zamani wa Libya Moammar Gadhafi kumkabidhi kwa maafisa wa Scottland ili kufikishwa mahakamani.

Al-Megrahi, alitumikia miaka minane ya kifungo chake cha maisha katika jela ya Uskochi kabla ya kuachiwa huru miaka mitatu iliyopita, kwa misingi ya kibinadamu, kutokana na kile madaktari walieleza ni ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo na kusema alikua na miezi mitatu kabla ya kufariki.

Al-Megrahi alikanusha kuhusika katika njama hiyo na alisema ushaidi mpya utasafisha jina lake.

Baadhi ya jamaa za waathiriwa wa Lockerbie nchini Uingereza wameeleza masikitiko yao kutokana na kifo cha al-Megrahi, wakisema wanaamini hakua na hatia, na alishtakiwa kwa makosa.

XS
SM
MD
LG