Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:07

Sanders na Clinton washiriki mdahalo wa New York


Wademocrat wanaowania uteuzi wa kugombea urais, Bernie Sanders and Hillary Clinton wakijibu maswali wakati wa mdahalo wa Alhamisi usiku.
Wademocrat wanaowania uteuzi wa kugombea urais, Bernie Sanders and Hillary Clinton wakijibu maswali wakati wa mdahalo wa Alhamisi usiku.

Wademocrat wanaowania uteuzi wa kugombea urais, Bernie Sanders, na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, walifanya mdahalo jana usiku uliokuwa na majibizano katika eneo la Brooklyn, New York kabla ya tukio muhimu la upigaji kura wa awali unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo huko New York.

Wawili hao walikuwa na majibizano makali kila mmoja akihoji maamuzi ya mwenzake. Sanders ambaye katika wiki za karibuni alisema haamini kwamba Clinton anastahili kuwa Rais, jana Alhamis alisema anakubali kwamba Clinton ana sifa za kuwa rais, lakini anahoji maamuzi yake.

Alizingumzia uungaji mkono wake kwa vita nchini Irak na kukubali kwake msaada wa fedha za kampeni kutoka mabenki na makampuni ya Wall Street.

Clinton naye aliishutumu kambi ya Sanders kwa kutoa maneno ya uongo dhidi yake. Clinton alisema watu wa New York walimchagua kuwa seneta mara mbili na Rais Barack Obama alimteuwa yeye kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

XS
SM
MD
LG