“Kuna njia mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo ukiachilia mbali mapambano ya kijeshi,” H.R McMaster amesema Jumamosi.
“Lakini ni kukimbizana kwa sababu anakaribia karibu zaidi na zaidi na hakuna muda uliosalia,” akimkusudia katika maelezo yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un," amesema.
Korea Kaskazini imetangaza wiki iliyopita kuwa hivi sasa inaweza kuipiga nchi ya Marekani kwa kombora, baada ya kufanya jaribio la kombora jipya la balistika lenye uwezo wa kufika katika mabara mengine.
Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa Pentagon inatizama maeneo ya magharibi mwa pwani ya Marekani ambako mifumo ya kujihami inaweza kuwekwa, kufuatia tishio la Korea Kaskazini kwamba itaipiga Marekani
Shirika la habari la Reuters limesema kuwa ulinzi huo wa kujihami utahusisha kuwekwa mitambo ya kuzuia makombora ya balistika yenye urefu kwenda juu kama ile iliyokuwa imewekwa Korea Kusini.