Taarifa ya kwanza iliyoripotiwa na gazeti la Washington Post kwamba rais alitoa siri za kiwango cha juu kuhusiana na mikakati ya kupambana na Kikundi cha Islamic State (ISIS) ni zauongo, McMaster aliwaambia waandishi wa habari katika ikulujana jumatatu.
McMaster aliongeza kwamba alikuwepo hapo na kitu kama hicho hakikutokea.
Rais hakutoa taarifa yoyote ya operesheni ya kijeshi ambayo ilikuwa haijafahamika kwa umma, aliongeza.
Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson alisema alihudhuria mkutano wa Mei 10 na waziri wa mambo ya nje wa Russia pamoja na balozi wa Russia nchini Marekani.
Tillerson aliunga mkono maelezo yaliyotolewa na McMaster, akiongeza katika taarifa yake kwamba mazungumzo yakina yaliyojadiliwa miongoni mwao yalikuwa juhudi za pamoja na vitisho kuhusu namna ya kukabiliana na ugaidi.