Kitendo hicho kinadaiwa kufanyika tarehe 31 Desemba katika klabu ya usiku mjini Barcelona, polisi wliliambia shirika la habari la Associated Press.
Alves sasa atafikishwa mbele ya jaji ambaye ataamua juu ya mashtaka hayo.
Shtaka la unyanyasaji wa kijinsia nchini Uhispania linaweza kumaanisha chochote kuanzia kupapasa kingono bila ridhaa ya mtu, kumshika kwa nguvu hadi ubakaji.
Polisi walisema hawakuweza kutoa maelezo zaidi kuhusu kesi hiyo.
Alves mwenye umri wa miaka 39 ni mmoja wa wachezaji waliofanikiwa zaidi katika kandanda, akishinda mataji makubwa na vilabu kadhaa vya juu vikiwemo Barcelona, Juventus na Paris Saint-Germain. Kwa sasa anachezea klabu ya Pumas ya Mexico.